
Malkia Elizabeth II, wa Uingereza alitawala kwa muda mrefu zaidi ambapo utawala wake ulidumu kwa miongo saba
Elizabeth aliingia madarakani mwaka 1952, baada ya kifo cha baba yake, Mfalme George VI.
Malkia Elizabeth II amefariki katika Kasri la Balmoral huko Scotland baada ya madaktari kusema walikuwa na wasiwasi kuhusu afya yake
Kutokana na kifo cha Malkia Elizabeth II wa Uingereza mwanae Prince Charles mwenye miaka 73 ataiongoza nchi katika maombolezo wakati akisubiri kuthibitishwa kuwa mfalme mpya