
Maombolezo hayo yataanza September 10,2022 hadi September 14,2022, katika kipindi chote cha maombolezo, bendera zote zitapepea nusu mlingoti nchini Tanzania zikiwemo kwenye Balozi za Tanzania
Katika taarifa ya Ikulu ya Tanzania imeeleza kuwa Rais Samia amewaomba Watanzania wote kuungana na wenzetu wa Uingereza katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na aliyekuwa Kiongozi wao nchini humo.