Alhamisi , 20th Oct , 2022

Mnyama anayejulikana kwa upole wake duniani Twiga, amemuua mtoto mwenye urmi wa miaka 16 kwenye hifadhi moja ya wanyama huko nchini Afrika Kusini katika shambulio lisilo la kawaida.

Habari zinasema kwamba mtoto huyo alikua ameambatana na mama yake mzazi mwenye umri wa miaka 25 kwenye hifadhi hiyo iliyopo kaskazini mwa KwaZulu-Natal baada ya kuvamiwa na Twiga huyo.  

Mtoto alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu na daktari aliyekua karibu, huku mama yake akikimbizwa hosptali akiwa kwenye hali mbaya.  

Polisi wa nchi hiyo wameanza uchunguzi wa tukio hilo. Matukio ya twiga kushambulia binadamu ni nadra sana kutokea duniani.