Jumanne , 1st Nov , 2022

Bunge limeazimia kwamba wanafunzi wote wenye vigezo vya kupata mikopo na hawajapata mikopo mpaka sasa, serikali iangalie utaratibu mzuri wa kuwawezesha wanafunzi hawa kupokelewa vyuoni ili waendelee na masomo yao wakati serikali ikitafuta fedha kwa ajili ya mikopo.

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson

Hyo yamejiri hii leo Novemba Mosi, 2022, mara baada ya mjadala kuibuka bungeni juu ya uwepo wa idadi kubwa ya wanafunzi wenye sifa za kupata mikopo ya elimu ya juu kukosa, jambo ambalo limefanya wengi kushindwa kuendelea na masomo.

Aidha wakati huo huo Spika wa Bunge hilo Dkt. Tulia Ackson, ameagiza Bodi ya Mikopo (HESLB)kufika mbele ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Novemba 4, mwaka huu, kujibu yanayowakabili mara baada ya kukataa kutoa ushirikiano kwa kamati iliyoundwa na Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda, kuchunguzwa kwa zoezi la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi.