Jumamosi , 19th Nov , 2022

Wadau mbalimbali wa siasa nchini wamepongeza uongozi wa Rais wa Zanzibar Dr Hussein Ali Mwinyi hasa kwa jinsi alivyoweza kudumisha amani na mshakamano ndani ya wananchi 

Katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao (Zoom) uliowakutanisha wadau mbalimbali wa masuala ya kisiasa wenye lengo la kujadili Tathmini ya Uongozi wa Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika kuimarisha Demokrasia Zanzibar na Kudumisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa wamesema kuwa kwa muda aliokaa madarakani amefanikiwa kuwaunganisha watanzania

Mwanasiasa Mkongwe nchini Baraka Shamte amesema amedumisha umoja wa kitaifa, ajira kwa vijana na kuwajali watumishi wa umma

"Rais Mwinyi ameweza kuwaunganisha wananchi wote wa Zanzibar kuwa kitu kimoja kwa kupitia serikali ya umoja wa kitaifa. amejitahidi kuhubiri mambo haya na kushirikisha ingawa kulikuwa na vipingamizi lakini ameweza kufanya jambo nchi imefanikiwa" 

"Rais Mwinyi amegawa bodaboda kwa vijana wetu wajasiriamali wa kaskazini Pemba na kusini Pemba, hizi zimewasaidia vijana wetu ambao walikuwa hawana ajira" 

"Rais Mwinyi ameweza kutengeneza mshahara wa watumishi wa serikali, amewaongeza zaidi ya asilimia 50, kama hiyo haitoshi anafikiria kwa sasa anashuhulikia wastaafu kupata nyingeza ya pensheni" amesema Baraka Shamte 
Kwa upande wake , Mwenyekiti taifa chama cha ADA TADEA Juma Ali Khatib ameeleza mchango wa vyama vya siasa hususani upinzani katika kuimarisha amani Zanzibar

"Vyama vya siasa vina mchango mkubwa katika kusimamia na kuleta maendeleo, upinzani sio uadui, upinzani ni kuweza kuisaidia serikali pale ambapo kwa serikali imetoa ahadi zake na kuweza kuboresha na kushirikiana na serikali"

"Tunapofanya uchaguzi tukimaliza Rais anayepatikana anakuwa wa watu wote, kwahiyo tumempata Rais mchapakazi na uchumi umeimarika na sisi vyama vya siasa tuna wajibu mkubwa wa kuleta maendeleo kupitia wanachama wetu" amesema mwanasiasa huyo

Makamu Mwenyekiti wa kampuni ya Jitegemee, Joseph Meza yeye amekemea baadhi ya wanasiasa wanaotumia neno wazanzibar kuwasemea mambo ambayo hawajasema akitolea mfano sakata la uteuzi wa mkurugenzi wa tume ya uchaguzi Zanzibar

"Rais Mwinyi alimteua Mkurugenzi wa tume ya  Uchaguzi, sasa watu wanahoji kwanini amemteua, na watu wanawaweka nyuma wazanzibar kuwa hawataki, sasa umewauliza saa ngapi, mtu ameteuliwa mchana jioni unasema wanzanzibar hawataki umewauliza saa ngapo ?"

"Kwenye vyama vingi nadhani ni suala la kuvumiliana na kushauriana, lakini hatuwezi kufikia popote ikiwa tuna hizo negative image" amesema mwanasiasa huyo

Katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia Makini Ameir Ameir amesema kuwa tangu serikali ya Rais Mwinyi iingie madarakani hakuna vurugu wala mabomu yaliyosikika zanzibar

"Tangu Rais Mwinyi aapishwe hatujasikia mabomu, wananchi kukamatwa, viongozi wa kisiasa kukamatwa wala uvunjifu wa amani, hii inaonesha dhahidi kuwa yeye kama Rais ametimiza wajibu wake kuhakikisha Zanzibar inakuwa na amani"

"Wazanzibar tusikubali kutumbishwa, Zanzibar sasa imekuwa ni njema na ina amani, tuhakikishe kwamba tunaungana kwa umoja wetu, na mimi niko tayari usiku na mchana kumsaidia Rais na niko tayari kusema lolote na kumwambia yeyote ambaye hana dhamira njema na Zanzibar" - Ameir Ameir, Katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia Makini 

Katika sekta ya habari Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri (TEF) Deodatus Balile ameeleza kuwa Rais Mwinyi amerejesha mawasiliano kati ya wananchi na serikali kupitia vyombo vya habari

"Rais Mwinyi amerejesha mawasiliano kati ya serikali na vyombo vya habari, na imeleta mawasiliano ya karibu kati ya serikali na wananchi, tangu ameingia amerejesha mikutano ya kila mwezi kukutana na wahariri na waandishi wa habari"