
Katika taarifa, wizara hiyo ilisema hakuna mshiriki katika mbio za marathon aliyewasilisha dalili zozote za virusi hivyo hatari.
Iliongeza kuwa hakuna kisa chochote cha Ebola kilichosajiliwa katika mji mkuu zaidi ya wale ambao tayari wako chini ya karantini.
Nchi hiyo inakabiliwa na mlipuko wa Ebola ambao hadi sasa umesababisha vifo vya zaidi ya watu 50. Shule zimefungwa na lockdown kuwekwa katika wilaya mbili zinazodhaniwa kuwa kitovu cha mlipuko.
Mamlaka zinasema juhudi zimefanywa kuzuia usafirishaji wa virusi hivyo kwenda maeneo mengine ya nchi.