Jumanne , 22nd Nov , 2022

Bodi ya maji bonde la Rufiji imeanza utekelezaji wa agizo la serikali la kuwaondoa wananchi waliovamia vyanzo vya maji  kwa kubomoa mifereji isiyo rasmi ambayo inachepusha  maji katika bonde la Ihefu na Usangu na kuathiri mtiririko wa maji katika mto Ruaha mkuu

Zoezi hilo ni kufuatia kauli ya  waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira  Selemani Jafo  aliyoitoa hivi karibuni  katika hifadhi ya taifa ya Ruaha mara baada ya kujionea mto Ruaha mkuu kukauka takribani miezi mitatu sasa na kupelekea athari kubwa kwa wanyama,na sasa

Utekelezaji wa zoezi hili  la kubomoa mifereji isiyo rasmi na kuchepusha maji linafanyika  katika bonde la usanga na ihefu wilayani Mbalali ambako kilimo cha umwagiliaji kimeendelea kushamiri na kuathiri mtiririko wa maji katika mto ruaha mkuu ambao ni tegemeo kwa wanyama katika hifadhi ya taifa ya Ruaha