Foleni ya magari katika eneo la Pandambili
Mashuhuda wamesema wananchi wamefunga barabara hiyo tangu saa 8:00 mchana wa leo Desemba 9, 2022, hali iliyopelekea kuwepo kwa foleni kubwa ya magari katika barabara hiyo.
Hadi sasa viongozi ikiwemo jeshi la polisi wamefika eneo hilo na wameweza kuwadhibiti wananchi na kuanza kuruhusu magari kutembea.
Juhudi za kumtafuta Mkuu wa wilaya ya Kongwa zinaendelea.