Jumanne , 14th Feb , 2023

Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko ya Mawaziri katika Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Makatibu wakuu wa Wizara hizo.

Kushoto ni Mohamed Mchengerwa aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili, Dkt Hassan Abbas, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Balozi Dkt. Pindi Chana, Waziri wa Michezo

Taarifa ya mabadiliko hayo imetolewa hii leo Februari 14, 2023, ambapo amemhamishia Dkt Hassan Abbas kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, ambapo hapo awali alikuwa ni Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Rais Samia pia amemhamishia Wizara ya Maliasili na Utalii Mohamed Mchengerwa, ambaye awali alikuwa ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, nafasi ambayo amehamishiwa Balozi Dkt. Pindi Chana.

Aidha Rais Samia amemteua Said Yakub, kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na uteuzi wa wote hao umeanza mara moja na wataapishwa kesho Februari 15, 2023.