Jumatano , 15th Oct , 2025

Kifo chake kimetokana na kupata mshtuko wa moyo wakati wa matembezi yake ya asubuhi kwenye chuo hicho.

Waziri Mkuu wa zamani na Mwanasiasa mkongwe na  mashuhuri wa Kenya Raila Amolo Odinga, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.

Raila ameaga dunia siku ya leo Jumatano Oktoba 15, 2025 alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya macho ya Ayurvedic-cum-research huko Koothattukulam katika wilaya ya Ernakulam ya Keralan nchini India.

Kifo chake kimetokana na kupata mshtuko wa moyo wakati wa matembezi yake ya asubuhi kwenye chuo hicho.

Kwa mujibu wa kituo hicho, Odinga ameaga dunia majira ya saa 3:52 asubuhi hii na amekuwa katika kituo hicho kwa siku tano mfululizo akitibiwa katika safari ambayo alikuwa ameambatana na mtoto wake aliyekuwa akitibiwa katika kituo hicho pamoja na daktari wake binafsi.

Amewahi kuwa Waziri Mkuu wa Kenya kati ya mwaka 2008 hadi 2013 enzi za uhai wake sambamba  na kufanya kampeni tano za kuwania urais—mwaka wa 1997, 2007, 2013, 2017, na 2022 ambazo zote ziliisha bila mafanikio. Mwili wake kwa sasa umehifadhiwa hospitalini, polisi wamesema.