Burundi kutumia dimba la Mkapa kufuzu AFCON
Timu ya taifa ya Burundi 'The Swallows' watakuwa wenyeji wa Cameroon katika mchezo wa Kundi C wa kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Tanzania.