Coastal Union Yahamia Arusha

Klabu ya Coastal Union ya mkoani Tanga imehamia mkoani Arusha na itatumia uwanja wa itaufanya uwanja wa Sheik Amri Abedi kuwa uwanja wake wa nyumbani kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania bara kipindi chote ambacho uwanja wa Mkwakwani unaendelea kufanyiwa matengenezo. Awali timu hiyo Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara mwaka 1988 ilikua inautumia uwanja wa KMC Complex kama uwanja wake wa nyumbani.
Coastal Union mabingwa wa zamani wa ligi ya Tanzania bara itatumia uwanja wa Sheikh Amri Abedi kama uwanja wake wa nyumbani baada ya awali kutumia uwanja wa KMC Complex, ligi kuu itakaporejea timu ya Wagosi wa Kaya au Wana Mangushi itakuwa Jijini Arusha.