"Morogoro ni mkoa wa kimkakati" - RC Malima
Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza kusambaza umeme kwenye vitongoji 166 vilivyopo mkoa wa Morogoro baada ya kukamilisha usambazaji wa nishati hiyo kwenye vijiji 652 kati ya 669 ikiwa ni sawa na asilimia 97.5.