Bashe apiga marufuku biashara ya Kangomba
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, amepiga marufuku wafanyabiashara wanaonunua kahawa kwa njia ya Kangomba na kuagiza wakamatwe huku akisisitiza kuwa uwekezaji mkubwa unaofanywa katika zao hilo umelenga kuteka soko la kahawa ya Tanzania kimataifa.