Stars vitani leo dhidi ya Congo DRC

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars leo Oktoba 10,2024 itashuka dimbani ugenini dhidi ya Congo DRC kweye mchezo wa kufuzu mashindano ya AFCON itakayofanyika nchini Morocco 2025. Stars itaingia kwenye mchezo huu ikichagizwa na urejeo wa Nahodha wa timu Mbwana Samatta ambaye alikosekana katika michezo miwili iliyopita ya timu ya taifa.
Taifa Stars imecheza michezo mitatu hivi karibuni dhidi ya Congo DRC Stars imefungwa mechi moja na kutoka sare michezo miwili, leo usiku majira ya saa moja usiku kwa majira ya Afrka Mashariki utapigwa mchezo wa kufuzu AFCON 2025 ugenini nchini Congo DRC katika uwanja wa Stade des Martyrs.