Hatujacheza vizuri lakini ninafuraha- Klopp
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amewasifu wachezaji wake kwa kupambana na Inter Milan na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini, huku akiweka wazi kuwa hawakucheza vizuri lakini wamefunga mabao mawili mazuri.

