Simba wanacheza mchezo wa 3 leo, ndani ya siku 10
Mabingwa wa Tanzania bara Simba SC wanashuka dimba leo jioni kucheza mchezo wa 3 mfululizo ugenini dhidi ya Kagera Suga katika dimba la Kaitaba huko Bukoba mkoani Kagera. Mchezo huu ni wa kiporo na unachezwa Saa 10 jioni.