Mvua kubwa kunyesha siku tatu mfululizo
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la uwepo wa mvua kubwa itakayonyesha hii leo Januari 17, 2022, katika baadhi ya maeneo huku athari zinazotajwa kutokea ni pamoja na shughuli za uchumi kusimama na makazi ya watu kujaa maji.