Wananchi Kigoma hatarini kwa kunywa maji machafu
Wananchi wa kijiji cha Mkwanga halmashauri ya wilaya ya Kigoma wanalazimika kuendelea kutumia maji machafu ya mto Kaseke baada ya mkandarasi anayesimamia na anayetekeleza mradi wa maji katika eneo hilo kushindwa kukamilisha maboresho ya mradi huo uliotakiwa kukamilishwa mwezi Mei 2021.

