Tanzanite yaweka kambi Arusha
Timu ya Taifa ya Tanzania ya wanawake chini ya miaka 20 ''Tanzanite'' imeondoka Zanzibar kuelekea Karatu mkoani Arusha kwa kambi ya maandalizi ya mchezo wa marudiano wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya timu ya taifa ya Ethiopia utakaochezwa mapema mwezi ujao.

