Tanzania yapokea msaada wa bilioni 119.2
Serikali ya Ujerumani imeipatia Tanzania msaada mwingine wa Euro milioni 45 sawa na takribani shilingi za Tanzania bilioni 119.2 kwa ajili ya kutekeleza miradi mitatu katika sekta za maji, afya na kuendeleza sekta ya maliasili na utalii.