Kilichomkuta Serena Williams ni huzuni
Mcheza tenisi anayeshika nafasi ya nane kwenye viwango vya ubora Duniani kwa mujibu wa Chama cha wacheza tenisi cha Wanawake Duniani, Serena Williams ameshindwa kuendelea na mchezo wake katika michuano ya Wimbledon usiku wa kuamkia leo baada ya kupata maumivu ya mguu.

