Wizara yataka kujua idadi ya vijiji vya Tanzania
Wizara ya Maji imesema inafanya mageuzi makubwa kwenye suala la maji na kwamba inataka kujua idadi ya vijiji vyote vilivyopo Tanzania, na kuvibaini vile ambavyo vimekwishapata maji na vile ambavyo havina maji safi na salama kwa lengo la kuhakikisha inaongeza nguvu katika usambazaji.

