Mbunge apendekeza bodaboda wafungiwe leseni zao
Mbunge wa Viti Maalum Neema Lugangira, ametoa pendekezo kwa serikali kuhusu faini ya bodaboda na bajaji kwamba waweke mifumo kwenye leseni za madereva hao utakaoruhusu dereva kulipa faini kwa makosa mawili pekee na akitenda kosa la tatu basi afungiwe leseni yake.

