Atakayetoa taarifa ya mhalifu Dar kulipwa Mil. 2
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limetangaza donge nono la kiasi cha shilingi milioni mbili kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa za kweli na kwa usiri mkubwa kwa jeshi hilo kuhusu mtu anayefanya uhalifu wa kutumia silaha, lengo likiwa ni kuhakikisha mkoa huo unabaki kuwa shwari.

