Yanga kuingia kambini kesho, tayari kwa mapambano
Kikosi cha mabingwa wa Kihistoria wa Tanzania bara Yanga SC kitaingia kambini kesho Jumatano Julai 7, 2021, tayari kwa maandalizi ya michezo miwili ya Ligi kuu na ule wa fainali ya kombe la FA dhidi ya watani zao Simba SC. Kikosi hicho kinarejea baada ya mapumziko ya siku nne.

