Kampeni ya Namthamini 2021 yazinduliwa rasmi
Ikiwa leo ni Siku ya Hedhi Salama Duniani, East Africa Television na East Africa Radio imezindua kampeni ya Namthamini kwa mwaka 2021, tayari kwa kukusanya taulo za kike (pedi) na kuzigawa kwa wanafunzi wa kike wenye uhitaji waliokatika mazingira magumu katika maeneo mbalimbali nchini.