Ukitumia 'fake name' tutakujua tu- Dkt.Ndugulile
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile, amewasisitiza Watanzania kuendelea kuhakiki namba zao za simu na kutumia mitandao vizuri ili kuepukana na wimbi la uhalifu wa mtandaoni ambao serikali inakabiliana nao kwa sasa.

