Bernard Morrison akwepa rungu la Bodi ya Ligi
Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Bernard Morrison amekwepa kufungiwa na kupingwa faini baada ya kumvuta bukta mshika kibendera kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Mwadui wa Ligi kuu Bara uliomalizika kwa simba kupata ushindi wa bao 1-0 juma lililopita mkoani Shinyanga.