Matola achimba mkwara, lakini alia na uchovu Simba
Kocha msaidizi wa klabu ya Simba, Selemani Matola amesema kucheza michezo mingi mfululizo katika kipindi kifupi kimechangia kuwafanya wachezaji wake kucheza na hali ya uchovu jambo aliloliona kwenye mchezo wa usiku wa jana waliopata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji.