Bunge lampitisha kwa kishindo Dkt. Mpango
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha kwa asilimia 100 jina la aliyekuwa Waziri wa Fedha Dkt. Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya jina lake kupendekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.