Maelfu wajitokeza kuuaga mwili wa Dk. Magufuli
Maelfu ya wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam, wakiongozwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, wamejitokeza kwa wingi kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli, aliyefariki dunia Machi 17, 2021, katika hospitali ya Mzena kwa tatizo la moyo.