Kenya kuomboleza siku saba kifo cha Magufuli
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ametangaza siku 7 za maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, kilichotokea jana Machi 17, 2021, na bendera ya nchi hiyo pamoja na ile ya Jumuiya ya Afrika Mashariki zitapepea nusu mlingoti.