Atakayepoteza Passport laki tano itamtoka
Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania imesema kuwa mtu atakayepoteza Pasi yake ya kusafiria (Passport), itamlazimu kutoa taarifa polisi pamoja na kutangaza kwenye gazeti na kwamba ni lazima atoe kiasi cha shilingi Laki Tano kwa kupoteza Passport hiyo, na ili aweze kupata nyingine.