Wizara ya Afya yasisitiza kuchukua tahadhari
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewashukuru Watanzania wote kwa kutekeleza agizo la Rais Dk. John Magufuli la maombi ya siku tatu kuliombea taifa dhidi ya janga la corona, na imewasisitizia Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa mbalimbali.