Polisi yatoa onyo wanaotaka kuandamana
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, CP Liberatus Sabas, amesema kuwa jeshi la polisi halitamvumilia mtu yeyote awe kiongozi wa chama au mfuasi, atakayefanya maandamano batili na kama kuna yeyote ambaye hakuridhika na matokeo afuate taratibu za kisheria kudai haki zao kama zipo.