Mchungaji Mwamposa asakwa na Polisi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Salum Hamduni, amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka Mtume Boniface Mwamposa, aliyetoweka baada ya watu takribani 20 kufariki, wakati wakikimbilia kukanyaga mafuta katika kongamano lake lililofanyika mkoani humo.