Mama wa Kabendera amuangukia Rais Magufuli
Mama Mzazi wa Mwandishi wa Habari, Erick Kabendera, anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, amemuangukia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, na kumuomba amsamehe mwanaye ili arudi nyumbani na kuendelea kumlea.