Katibu Mkuu wa Chama cha CCK adakwa na TAKUKURU
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Ilala, inamshikilia Katibu Mkuu wa Chama cha siasa cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi, kwa makosa ya kujifanya ni Ofisa wa Serikali na kuomba rushwa ya kiasi cha Shilingi milioni 50, kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya BECCO.