Wababe hawa wamefuzu nusu fainali CWC
Baada ya Real Madrid kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali katika michuano ya Klabu ya dunia kwa magoli 3-2 dhidi ya Borussia Dortmund huku wakiwa pungufu baada Dean Huijsen kutolewa nje kwa kadi nyekundu, rasmi sasa Los Blancos watakutana na PSG katika hatua hiyo.