Aliyemuokoa Tundu Lissu ateuliwa na Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, leo amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kuteua Mawaziri, Makatibu wakuu na Balozi, ambapo miongoni mwa watu walioteuliwa ni daktari aliyeongoza timu ya matabibu kumuokoa Tundu Lissu alipopigwa Risasi mwaka 2017.