Chanzo cha ajali iliyoua watu 15 Mara
Takribani watu 15 wamefariki dunia baada ya kuteketea kwa moto kufuatia ajali mbaya iliyotokea katika eneo la Komaswa maarufu kama kwa Gachuma lililopo wilayani Tarime mkoani Mara kwa kuzikutanisha gari mbili za abiria aina ya Toyota Hiace kugongana uso kwa uso na kisha kuteketea kwa moto.