Bulaya 'aibuka' tena, sakata la pesa za wastaafu
Waziri Kivuli wa Sera, Bunge, Kazi Vijana na Ajira, na Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya ameendelea kuikalia kooni Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii SSRA, akidai kuwa kikokotoo kitakachotumika Tanzania ni kikubwa kuliko nchi zingine za Afrika Mashariki.