Waziri Kangi Lugola akifanya ukaguzi wa kiwanda cha samani cha Jeshi la Magereza Jijini Arusha
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola ameliagiza Jeshi la Magereza mkoani Arusha kuanza upya ujenzi wa kiwanda cha kisasa cha samani cha jeshi hilo ambacho kiliungua moto mwezi uliopita.