Ummy azitaka halmashauri na miji kujitathmini
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu amezitaka Halmashauri za Miji, Majiji, Wilaya, Vitongoji na Vijiji zilizofanya vibaya katika mashindano ya afya na usafi wa mazingira kujitathmini na kuweka mikakati madhubuti ya utunzaji wa mazingira.