Wasomali wapinga Israel kuitambua Somaliland
Umati mkubwa ulikusanyika katika mji mkuu Mogadishu, ndani ya uwanja wa taifa, ambako viongozi wa kidini waliongoza maandamano yaliyotoa wito wa umoja wa kitaifa na kulaani hatua hiyo wakisema ni shambulio dhidi ya uhuru na umoja wa ardhi ya Somalia.

