Jela miaka 20 kisa nyama ya Nguruwe pori
Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi imemhukumu Sweetbert Lyankuba (41) mkazi wa Mamba kutumikia kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na nyara za serikali nyama ya mnyamapori Nguruwe kiasi cha kilogramu 420.

