Kocha Mwadui FC, afariki dunia
Kocha msaidizi wa Klabu ya Mwadui Jumanne Ntambi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo huko Mkoani Shinyanga, huku chanzo cha kifo chake kikidaiwa ni kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu alilokuwa akisumbuliwa nalo kwa kipindi kirefu.