Simbachawene asema mtumishi hajilimbikizii mali
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, amesema kwenye utumishi wa umma sio sehemu ya kuvuna utajiri na kujilimbikizia mali bali ni kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa umma.