DC Pangani ataka watumishi wa siku nyingi watolewe
Mkuu wa wilaya ya Pangani, Zainabu Abdallah amekiomba Chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na Wizara husika, kuwahamisha watumishi waliokaa muda mrefu katika wilaya hiyo ambao baadhi yao hawatekelezi majukumu yao na badala yake wamekuwa wakifanya kazi zao binafsi.